Idara za Chama

Chama kina Sekretariati ya Chama katika kila ngazi; za Taifa, Jimbo, Kata/Wadi na Tawi.

Katika ngazi ya Taifa kutakuwa na Sekretariati katika Makao Makuu ya Chama Dar Es Salaam na katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Tanzania Zanzibar.

Sekretariati ya kila ngazi itakuwa na idara zifuatazo:-

1. Idara ya Oganaizesheni na Utawala

2. Idara ya Fedha, Uchumi na Mipango

3. Idara ya Itikadi, Sera, Utafiti na Mafunzo

4. Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma

5. Idara ya Mambo ya nje ya Chama

6. Idara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu

7. Idara ya Kampeni na Uchaguzi na

8. Idara ya Taasisi za Dola na Vyombo vya Uwakilishi