Haki na Wajibu wa Mwanachama
Haki za Mwanachama:
Kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa Chama wa ngazi yoyote kwa mujibu wa taratibu za Chama.
Kupata habari zote zilizojadiliwa na kutolewa uamuzi na wanachama katika kumbukumbu za vikao vinavyomhusu.
Kutoa hoja za kusahihisha na kuweka sawa maongozi ya Chama bila hofu wala upendeleo. Hoja zitatolewa kwa kuwasilishwa kwa maandishi kwa Katibu wa Chama wa ngazi inayomhusu moja kwa moja na mtoa hoja.
Kuwa na haki ya kujitetea mbele ya kikao cha Chama kinachohusika katika mashtaka au madai yoyote; na kuwa na haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo mhusika hakuridhika na uamuzi wa kikao cha chini.
Wajibu wa Mwanachama:
- Kulipa ada za kila mwezi ili kufanikisha shughuli za Chama.
- Kujitoa mhanga kufanya shuguli za Chama bila kutegemea malipo na kuwa tayari kuchanga fedha na mali kukijenga na kukiimarisha Chama.
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli na uongozi wa Chama na kueneza sera na programu ya Chama.
- Kukuza moyo wa ushirikiano na kuheshimu uamuzi wa pamoja.
- Kuwa mwaminifu na mwadilifu kwa kusema na kutenda mambo ya kujenga na kukitukuza Chama.
- Kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu, kupinga uonevu, udhalimu, rushwa na ubaguzi wa kila aina na matendo yanayoharibu maadili ya jamii.
- Kujielimisha juu ya masuala ya jamii, kuelewa matatizo ya watu na kiini cha matatizo hayo na kujitahidi kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo kwa kushirikiana na wanaohusika.
- Kukilinda Chama dhidi ya mitafaruku, majungu na vitendo vya kukigawa na kukidhoofisha Chama