Pamoja Tutashinda

KATIBA YA CHAMA CHA NCCR – MAGEUZI

YA MWAKA 1992

Hii ni Katiba ya Chama cha NCCR – Mageuzi ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kuchapishwa katika matoleo yafuatayo:

Toleo la Kwanza                                1992

Toleo la Pili                                        1994

Toleo la Tatu                                      1995

Toleo la Nne                                       1999

Toleo la Tano                                     2000

Toleo la Sita                                        2002

Toleo la Saba                                      2014

UTANGULIZI

KWA KUWA NCCR – MAGEUZI ni chama cha siasa kinachotokana na harakati za Watanzania za kuigeuza jamii na mfumo mkongwe na wa kidikteta wa chama kimoja, na kujenga jamii mpya inayozingatia demokrasia ya jamii isiyo na mipaka au ufinyu wa vyamavya siasa; na

KWA KUWA mfumo wa Chama kimoja ulivinja nguvu za umma za kujiletea maendeleo na badala yake ukapandikiza uzembe wa mali na raslimaliza taifa, walafi wa utajiri na wakandamizaji wa umma wa wananchi; na

KWA KUWA NCCR-MAGEUZI inaamini na kutambua wazi kwamba, nchi yetu ina utajiri na rasilimali za kutosha kukidhi haja ya maendeleo ya jamii na mahitaji ya watu wake, kinyume cha hali iliyopo sasa ya kuendelea kuwa fukara siku hadi siku kutokana na mfumo mbaya wa siasa na uchumi wa Chama tawala na Serikali, mfumo usiojali mawazo, mchango, matakwa na masilahi ya wananchi walio wengi; na

KWA KUWA hadi kufikia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini watu mbali mbali walioshiriki na kujitoa mhanga, kiasi cha baadhi yao kuwekwa kizuizini, kulazimika kuwa wakimbizi wa kisiasa nje ya nchi, kutumikia kifungo na kupoteza kazi ili sudi ya mageuzi ya kulikomboa Taifa na hasa umma wa wanyonge ifanikiwe; na

KWA KUWA malengo ya sudi ya mageuzi ni kuwakomboa wanyonge na kujenga jamii mpya yenye kulinda na kutetea haki za binadamu, demokrasia ya kijamii isiyo na mipaka au ufinyu wa vyama vya siasa, usawa na haki kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisheria; na

KWA KUWA NCCR-MAGEUZI inaamini kuwa njia bora ya kuleta mageuzi na kuongoza Serikali katika kuleta mabadiliko haya katika jamii yetu ni kwa amani, hiari na nguvu ya hoja itokanayo na itikadi ya sera zetu zinazolenga kuwakomboa wanyonge na kuwaongoza wapate maendeleo na ustawi;

HIVYO BASI, Wanachama wa Chama cha NCCR-MAGEUZI, kupitia wawakilishi wetu kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa, tunathibitisha na kupitisha marekenisho ya Saba ya Katiba ya mwaka 1992, leo tarehe 18 January 2014, jijini Dar es Salaam.

SURA YA KWANZA
JINA, BENDERA NEMBO, MAKAO MAKUU, ITIKADI NA LUGHA RASMI.

1. JINA LA CHAMA litakuwa NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM – MAGEUZI; kwa kifupi NCCR-MAGEUZI.

Tafsiri yake kwa Kiswahili ni Chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa

2. BENDERA YA CHAMA itakuwa na rangi kuu mbili ambazo ni bluu na nyeupe. Rangi nyeupe na mashuke yaliyopo kila upande wa nembo, vina maana ya amani. Rangi ya bluu ina maana ya utajiri tulionao katika mito, maziwa, bahari, pamoja na utajiri wa rasilimali nyingine nyingi zilizopo nchini mwetu.

3. NEMBO YA CHAMA itakuwa na alama kuu ambazo ni picha ya mwanamke anayesoma kitabu, ikiwa na maana ya umuhimu wa elimu na maarifa, nyingine ni picha ya mwanamume anayelima kwa trekta, ikimaanisha umuhimu wa matumizi ya tekinolojia ya kisasa katika uzalishaji mali na utoaji huduma, pia chini ya picha hizo kutakuwa na utepe wenye maneno “Demokrasia na Maendeleo” ndani yake.

4. MAKAO MAKUU YA CHAMA yatakuwa Dar es Salaam na ofisi nyingine ndogo ya makao makuu itakuwa Zanzibar.

5. ITIKADI YA CHAMA ni UTU ambayo misingi yake ni udugu, maadili, usawa, haki, imani, mabadiliko, uhuru, wajibu, asili, kazi na endelezo.

6. LUGHA RASMI ya Chama itakuwa Kiswahili na Kingereza.

SURA YA PILI
MISINGI YA KISIASA NA MADHUMUNI YA CHAMA

7. Misingi ya Kisiasa ya Chama:

Misingi ya kisiasa ya Chama ni kama ifuatavyo:-

(1) Kukubali itikadi ya utu ambayo lengi lake ni ujenzi wa jamii yenye uhuru, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji, haki za binadamu, usawa na ustawi wa jamii inayokubali kutegemeana kwa binadamu katika msingi wa mmoja kwa wote na wote kwa mmoja.

(2) Kukubali na kuheshimu demokrasia ya vyama vingi vya siasa kama hatua iliyofikiwa katika mapambano ya kuleta demokrasia ya kijamii nchini na pia kuheshimu mchango wa vyama na vikundi vingine vya kijamii katika kukuza na kudumisha demokrasia ya kweli.

(3) Kukubali na kuheshimu usawa na haki ya kila mtu kisiasa, kiuchumi, kisheria na kijamii.

(4) Kukubali haki ya wanyonge kupewa upendeleo maalum ili waweze kujiendeleza kwa kasi zaidi.

(5) Kuheshimu kazi na shughuli halali za watu binafsi katika Nyanja zote za jamii na uchumi.

(6) Kupenda kushirikiana na watu, jamii na vyama vyenye kuamini na kutetea itikadi na au madhumuni yanayoshabihiana na yale ya Chama chetu.

8. Madhumuni ya Chama:

Madhumuni ya NCCR – MAGEUZI yatakuwa kama ifuatavyo:-

(1) Kutwaa hatamu za dola na kujenga jamii yenye demokrasia na maendeleo.

(2) Kuwa na utawala unaoheshimu Katiba na sheria.

(3) Kuwa na Bunge huru lenye mamlaka ya kuisimamia Serikali na vyombo vyake, linaloshirikisha wananchi na kuwajibika kwao.

(4) Kuwa na Mahakama huru zenye mamlaka ya kulinda haki za binadamu na haki za kisheria za wananchi.

(5) Kuwa na jamii inayoamini katika kufungamana kwa demokrasia na maendeleo.

(6) Kuwepo nafasi sawa kati ya mtu binafsi na jamii ya kujiendeleza kiuchumi na kijamii bila ya masilahi ya upande mmoja kupewa upendeleo usio wa halali kisheria.

(7) Kuwa na uchumi imara unaowanufaisha wananchi kwa njia ya soko, sekta binafsi, ushirika na sekta ya dola.

(8) Kuhakikisha kuwa lengo kuu la dola katika maendeleo ya nchi la kumwezesha kila mwananchi mwenye iwezo wa kufanya kazi kujipatia mahitaji na huduma muhimu linatekelezwa kwa kujibu wa Katiba hii, sera na program za Chama.

(9) Kutoa kipaumbele au upendelei wa makusudi kwa wananchi ambao wako nyuma kimaendeleo kwa Sababu zilizo nje ya uwezo wao ili kuinua maisha yao.

(10) Kuwa na sekta huru ya habari ambayo ina vyombo huru vya habari vyenye haki ya kupata na kusambaza habari bila woga.

(11) Kuwepo haki ya mtu binafsi kumiliki mali iliyopatikana kwa njia halali.

(12) Kuwepo mazingira safi na salama kwa ajili ya uhai wa binadamu na viumbe vingine.

(13) Kuwa na jamii isiyo na ubaguzi wa rangi, kabila, dini au jinsia na kuhakikisha panakuwepo usawa na haki kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika Nyanja zote za kimaisha.

(14) Kuwa na mipango ya maendeleo ya jamii inayozingatia mahitaji maalum ya walemavu ili kuwawezesha kuishi na kushiriki katika shughuli mbali mbali sawa na wanajamii wengine.

(15) Kuzingatia na kulinda haki na masilahi ya watoto katika jamii.

(16) Kuwa na mipango ya kuendeleza na kulinda haki na masilahi ya wazee katika jamii.

(17) Kujenga jamii inayozingatia kuwa vijana ni Taifa la leo.

(18) Kuwepo mfumo bora wa uchumi duniani uliojengeka katika misingi ya usawa na unaolinda haki ya nchi change kuendelea.

SURA YA TATU
UANACHAMA

9. Kujiunga na Chama:

Anayetaka uanachama anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-

(1) Awe ni raia wa Tanzania.

(2) Awe na umri usiopungua miaka kumi na nane.

(3) Awe na akili timamu.

(4) Awe anakubali itikadi, misingi ya kisiasa, madhumuni, sera, kanuni na taratibu za Chama.

(5) Akikubaliwa anunue kadi, alipe ada za Chama na kuorodheshwa katika daftari la orodha ya wanachama.

10. Haki za mwanachama:

(1) Kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa Chana wa ngazi yeyote.

(2) Kupata habari zote zilizojadiliwa na kutolewa uamuzi na wanachama katika kumbukumbu za vikao vinavyomhusu.

(3) Kutoa hoja za kusahihisha na kuweka sawa maongozi ya Chama bila hofu wala uoendeleo. Hoja zitatolewa kwa kuwasilishwa kwa maandishi kwa Katibu wa Chama wa ngazi inayomhusu moja kwa moja na mtoa hoja.

(4) Kuwa na haki ya kujitetea mbeke ya kikao cha Chama kinachohusika katika mashtaka au madai yeyote na kuwa na haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo mhusika hakuridhika na uamuzi wa kikao cha chini.

11. Wajubu wa mwanachama:

(1) Kulipa ada za kila mwezi ili kufanikisha shughuli za Chama.

(2) Kijitoa mhanga kufanya shuguli za Chama bila kutegemra malipo na kuwa tayari kuchanga fedha na mali kukijenga na kukiimarisha Chama.

(3) Kushiriki kikamilifu katika shughuli na uongozi wa Chama na kueneza sera na program ya Chama.

(4) Kukuza moyo wa ushirikiano na kuheshimu uamuzi wa pamoja.

(5) Kuwa mwaminifu na mwadilifu kwa kusema na kutenda mambo ya kujenga na kukitukuza Chama.

(6) Kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu, kupinga uonevu, udhalimu, rushwa na ubaguzi wa kila aina na matendo yanayoharibu maadili ya jamii.

(7) Kujielimisha juu ya masuala ya jamii, kuelewa matatizo ya watu na kiini cha matatizo hayo na kujitahidi kutafuta majibu ya matatizo hayo kwa kushirikiana na wanaohusika.

(8) Kukilinda Chama dhidi ya mitafaruku, majungu na vitendo vya kukigawa na kukidhoofisha Chama.

12. Kuondoka katika Chama:

Uanachama wa mtu utakoma kama moja ya mambo yafuatayo yatatokea:-

(1) Kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe.

(2) Kwa kufukuzwa baada ya kukiuka Katiba, kanuni, taratibu na maadili ya Chama.

(3) Kwa kujiunga na Chama kingine cha siasa.

(4) Kwa kufariki dunia.

SURA YA NNE
UONGOZI KATIKA CHAMA

13. Sifa za Kiongozi:

(1) Awe anajua kusoma na kuandika, anaheshimu, anatetea Katiba na kueneza itikadi na sera za Chama.

(2) Awe mchapakazi na mwenye uwezo wa kuongoza.

(3) Awe mwadilifu, mkweli kwa maneno na matendo, mtetezi na mpenda haki asiye na historia ya uhalifu na awe anaheshimu watu na mwenye kuaminika na kukubalika.

(4) Awe na upeo mpana kiakili na kuwa tayari kujiendeleza yeye binafsi kielimu na kutumia elimu aliyoipata kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.

(5) Awe na moyo na uwezo wa kufanya kazi na makundi mbali mbali ya jamii katika mazingira yoyote.

(6) Awe mtu aliye mstari wa mbele katika kujua matatizo ya jamii na kuyatafutia ufumbuzi.

(7) Awe ni mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake na awe na ufhujaa na ushupavu wa kutetea masuala ya msingi yanayogusa wanyonge na masilahi ya Taifa.

(8) Awe mtu mwenye msimamo wa kukipenda na kukifia Chama, asiwe kigeugeu, mwenye tams na mbabaishaji wa kisiasa na kimaish.

(9) Awe mtii na mwenye nidhamu ya Chama ya kuheshimu vikao, viongozi wenzake, wanachama na wananchi.

(10) Awe tayari kukosolewa pale anapokuwa na upungufu na awe tayarikujirekebisha.

14. Haki za Kiongozi:

Kiongozi atakuwa na haki zifuatazo:-

(1) Kujitetea kwenye kikao kinachoamua tuhuma dhidi yake.

(2) Kupinga hatua ya kufukuzwa uongozi kwa kukata rufaa kwenye kikao cha juu iwapo hakuridhika na uamuzi wa kikao cha chini.

15. Kuacha uongozi:

Kiongozi ataacha uongozi ikiwa moja ya mambo yafuatayo yakitokea;-

(1) Muda wa uongozi kumalizika.

(2) Kujiuzulu mwenyewekwa sababu binafsi.

(3) Kujiuzulu iwapo wale anaowaongoza wameishiwa imani na uongozi wake.

(4) Kufukuzwa au kuachishwa iwapo kiongozi amekiuka Katiba, kanuni, taratibu, maadili na sera za Chama.

(5) Kupatikana na hatia mahakamani kwa kosa ambalo Chama kitaona halistahili kutendwa na kiongozi wa Chama.

(6) Kupata maradhi yanayoondoa uwezo wa kufanya kazi.

(7) Kufariki dunia.

SURA YA TANO
VIKAO VYA CHAMA

16. Muundo wa vikao vya Chama:

Vikao vya Chama vitakuwa na muundo ufuatao:-

(1) Shina

(2) Kitongoji

(3) Tawi

(4) Kata/Wadi

(5) Jimbo

(6) Taifa

17. Shina

(1) Litakuwa popote walipo wanachama wasiopungua watano.

(2) Litakuwa na kikao kimoja ambacho ni Mkutano wa Shina.

(3) Wajumbe wa Mkutano wa Shina watakuwa:-

     (a) Mwenyekiti wa Shina (Balozi).

     (b) Katibu wa Shina

     (c) Wanachama wote waliopo katika Shina.

(4) Kazi za Mkutano wa Shina.

     (a) Kumchagua Mwenyekiti wa Shina (Balozi) unapofika wakati wa uchaguzi.

     (b) Kusimamia shughuli za Chama katika Shina.

     (c) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama ya Shina.

    (d) Kutekeleza maamuzi na maelekezo ya kikao cha juu yake.

     (e) Mkutano wa Shina utafanyika angalau mara moja kila mwezi.

(5) Kazi za Mwenyekiti wa Shina (Balozi)

     (a) Atakuwa msimamizi Mkuu wa shughuli za kila siku za Chama katika Shina.

     (b) Atakuwa msemaji na mhamasishaji Mkuu wa Chama katika Shina.

     (c) Ataongoza mikutano ys Shina.

(6) Kazi za Katibu wa Shida

     (a) Atakuwa mtendaji Mkuu wa Shina.

     (b) Atatunza daftari la orodha na kumbukumbu za wanachama waliopo katika Shina.

    (c) Atakusanya ada na mapato mengine ya Chama na kuyawasilisha kwa Katibu wa kitongoji baada ya kutoa stakabadhi ya malipo yaliyopokewa.

    (d) Atakuwa mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika Shina.

    (e) Atawajibika na kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika Shina kwa ngazi ya Kitongoji.

18. Kitongoji.

(1) Kitaundwa na Mashina yote yaliyopo katika Kitongoji.

(2) Kitakuwa na kikao kimoja ambacho ni Mkutano wa Kitongoji.

(3) Wajumbe wa Mkutano wa Kitongoji:-

     (a) Mwenyekiti

     (b) Katibu

     (c) Wanachama wote waliopo katika Kitongoji.

(4) Kazi ya Mkutano Mkuu wa Kitongoji.

     (a) Kumchagua Mwenyekiti wa Kitongoji.   

     (b) Kusimamia shughuli za Chama katika Kitongoji.

     (c) Kutekeleza maazimio na maelekezo ya kikao cha juu yake.

     (d) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama katika kitongoji.

     (e) Mkutano mkuu wa Kitongoji utafanyika angalau mara moja kwa mwezi.

(5) Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji

     (a) Atakuwa msimamizi Mkuu wa shughuli za kila siku za Chama katika Kitongoji.

     (b) Atakuwa msemaji na mhamasishaji Mkuu wa Chama katika Kitongoji.

     (c) Ataongoza mikutano yote ya Kitongoji.

(6) Kazi za Katibu wa Kitongoji

     (a) Atakuwa mtendaji Mkuu wa Kitongoji.

     (b) Atatunza daftari la orodha na kumbukumbu za wanachama waliopo katika Kitongoji.

     (c) Atakusanya ada na mapato mengine ya Chama na kuyawasilisha kwa Mweka Hazina wa Tawi    baada ya kutoa stakabadhi ya malipo yaliyopokewa.

     (d) Atakuwa mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika Kitongoji.

     (e) Atawajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika kitongoji kwa ngazi  ya Tawi.

19. Tawi

(1) Kutakuwa na Tawi katika kila eneo la Serikali ya Mtaa kwa mijini na Tawi katika kila eneo la Serikali ya Kijiji au mahali pengine popote kwa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(2) Vikao vya Tawi:

     (a) Mkutano Mkuu wa Tawi.

     (b) Kamati ya Tawi.

(3) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawi:

     (a) Mwenyekiti wa Tawi.

     (b) Katibu wa Tawi.

     (c) Mweka Hazina wa Tawi.

    (d) Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji na Katibu wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa/Kijiji waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi au Mwenyekiti na Katibu wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa/Kijiji waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi iwapo hakuna Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi.

     (e) Wenyeviti wa Chama wa Vitongoji.

     (f) Wenyeviti wa Serikali za Vitongoji waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

     (g) Wenyeviti na Makatibu wa vitengo vya Chama ngazi ya Tawi.

     (h) Wenyeviti wa Mashina (Mabalozi).

     (i) Wanachama wote waliopo katika Tawi.

(4) Kazi za Mkutano Mkuu wa Tawi:

     (a) Kumchagua Mwenyekiti wa Tawi unapofika wakati wa uchaguzi.

     (b)Kumchagua Mweka Hazina wa Tawi.

     (c) Kupokea taarifa ya Kamati ya Tawi.

     (d) Mkutano Mkuu wa Tawi utafanyika angalau mara moja kila baada ya miezi sita.

(5) Wajumbe wa Kamati ya Tawi:

      (a) Mwenyekiti wa Tawi.

      (b) Katibu wa Tawi.

      (c) Mweka Hazina wa Tawi.

     (d) Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji na Katibu wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa/Kijiji waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCT-Mageuzi.

    (e) Mwenyekiti na Katibu wa wajumbe wa  Serikali ya Mtaa/Kijiji waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi iwapo waliotajwa katika (d) ya ibara ndigo hii hawapo.

     (f) Wenyeviti wa Chama wa Vitongoji.

     (g) Wenyeviti wa Serikali za Vitongoji vilivyopo katika Tawi waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

     (h) Wenyeviti na Makatibu wa vitengo vya Chama vilivyopo katika Tawi hilo.

      (i) Wenyeviti wa Mashina (Mabalozi) waliopo vilivyopo katika Tawi hilo, isipokuwa wale ambao idadi ya                             wanachama wao ni chini ya watano.

(6) Kazi za Kamati ya Tawi:

       (a) Kuunda Sekretarieti ya Chama ya Kamati ya Tawi.

       (b) Kuendesha shughuli za kila siku za Chama,

       (c) Kusimamia utekelezaji wa sera za Chama,

       (d) Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato ya Tawi na miradi ya Chama.

       (e) Kusimamia matumizi ya fedha katika shughuli za Chama.

       (f) Kuwasilisha mawazo ya wanachama kwa wananchi.

       (g) Kuwahimiza wanachama kujiandikisha, kufanya kampeni na kuhakikisha kuwa Chama kinapata ushindi.

       (h) Kuwaandaa wanachama kushirikiana na wananchi wengine katika kuleta demokrasia ya kweli na maendeleo kwa kushirikiana na vyama vya kijamii.

       (i) Kutafuta wanachama wapya.

         (j) Kusimamia ustawi wa Mashina yaliyopo katika Tawi hilo.

         (k) Kujadili maombi na kuteuawagombea uongozi wa Chama ngazi za Vitongoji na Mashina.

         (l) Kumchagua Mweka Hazina wa Tawi.

        (m) Kuandaa Mkutano Mkuu wa Tawi.    

         (n) Kuongoza harakati za kupinga uonevu unaoweza kufanywa na Serikali au kikundi    chochote.

         (o) Kuwaelekeza wananchi jinsi ya kupata, kutetea na kulinda kazi zao.

         (p) Kushughulika na nidhamu ya viongozi na wanachama wa Tawi hilo na kuchukua hatua za kinidhamu                               isipokuwa kufukuza uanachama.

           (q) Kumjulisha aliyejiuzulu au kufukuzwa uanachama na ambaye ameomba kurudi katika Chama na kutoa                           mapendekezo kwa Kamati ya Kata/shehia.

          (r) Kujadili maombi ya wanaoomba kugombea uongozi wa Serikali za Mitaa na kuyawasilisha kwa Katibu wa                      Kata/Shehia wa Chama.

            (s) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama ya Tawi.

            (t) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya kila mwaka ya maendeleo ya kila kitengo cha Chama.

           (u) Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika katiba hii.

            (v) Kamati ya Tawi itakutana angalau mara moja katika kila miezi mitatu.

(7) Kazi ya Mwenyekiti wa Tawi:-

        (a) Atakuwa msimamizi Mkuu wa shughuli za kila siku za  Chama katika Tawi.

        (b) Atakuwa msemaji na mhamasishaji Mkuu wa Chama katika Tawi.

        (c) Ataongoza vikao vya Chama vya Tawi.

(8) Kazi ya Katibu wa Tawi:-

           (a) Atakuwa mtendaji Mkuu wa Chama katika Tawi.

          (b)  Atatunza daftari la orodha na kumbukumbu za Vitongiji na wanachama waliopo katika Vitongoji vya Tawi hilo.

         (c) Atatunza kumbukumbu na mali za Chama zisizoondosheka na zinazoondosheka na kumbukumbu nyingine muhimu.

          (d) Atasimamia vyanzo vya mapato na miradi ya Chama aliyopo katika Tawi hilo.

          (e) Atakuwa mdhibiti Mkuu wa mali za Chama za Tawi.

          (f) Atawajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa kazi za Chama katika Tawi kwa ngazi ya                          Kata/Shehia.

         (g)  Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

(9) Kazi ya Mweka Hazina wa Tawi:-

        (a) Atabuni/atatafuta fedha kwa ajili ya Chama.

        (b) Ataweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya Chama,

        (c) Ataandaa bajeti ya Chama.

        (d) Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya Chama.

20. Kata/Wadi.

(1) Kata/Wadi itakuwa na kikao cha Kamati ya Kata/Wadi.

(2) Wajumbe wa Kamati ya Kata/Wadi.

       (a) Mwenyekiti wa Kata/wadi

      (b) Katubu Kata/Wadi

      (c) Mweka Hazina Kata/wadi

     (d) Diwani wa Kata/Wadi hiyo aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

     (e) Wenyeviti wa Matawi yaliyopo katika Kata/Wadi

     (f) Wenyeviti wa Serikali za Mitaa/Vijiji na Makatibu wa wajumbe wa Serikali za Mitaa/Vijiji vya Kata/Wadi hiyo             waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

     (g) Wenyeviti wa Serikali za Mitaa/Vijiji na Makatibu wa wajumbe wa Serikali za Mitaa/Vijiji vya Kata/Wadi hiyo             waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi iwapo waliotajwa katika (f) ya ibara ndogo hii hawapo.

     (h) Wenyeviti na Makatibu wa vitengo vya Chama vya Kata/Wadi hiyo.

     (i) Katibu wa kitengo cha wanawake wa Kata/Wadi hiyo.

     (j) Wanawake Wenyeviti wa Vitongoji vya Kata/Wadi hiyo waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

(3) Kazi za Kamati ya Kata/Wadi:

      (a) Kumchagua na Mweka Hazina wa Kata/Wadi unapofika wakati wa uchaguzi.

      (b) Kuunda Sekretarieti ya kamati ya Kata/Wadi.

    (c) Kuwajadili waliojiuzulu au kufukuzwa uanachama na wanao omba kurudi katika Chama na kutoa                                     mapendekezo kwa Kamati ya Utendaji ya Jimbo.

    (d) Kujadili maombi na kuteua wagombea wa nafasi za uongozi katika marawi ya Chama yaliyopo katika Kata/Wadi hiyo.

    (e) Kujadili maombi na kuteua wagombea wa nafasi za uongozi katika matawi ya Chama yaliyopo katika  Kata/Wadi

    (f) Kujadili maombi na kutoa mapendekezo kuhusu wanaoomba kugombea udiwani na kuyawasilisha kwa Katibu wa Chama wa Jimbo. 

      (g) Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Chama katika Kata/Wadi hiyo.

      (h) Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato na miradi ya Chama.

      (i) Kusimamia matumizi ya fedha za Chama katika Kata/Wadi.

      (j) Kutoa mikakati na miongozo kuhusu maendeleo ya Chama katika Kata/Wadi hiyo.

      (k) Kupima utekelezaji wa shughuli za matawi ya Chama katika Kata/Wadi hiyo.

      (l) Kushugulikia nidhamu ya viongozi na wanachama wa Kata/Wadi hiyo na kuwachukulia hatua za kinidhamu isipokuwa kuwafukuza uanachama.

      (m) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za wanachama na viongozi kutoka katika matawi ya Chama ya                        Kata/Wadi hiyo.

      (n) Kubuni mikakati na kuhamasisha kwa shabaha ya Chama kupata kuungwa mkono na watu.

     (o) Kuhamasisha wanachama kugombea uongozi, kujiandikisha, kufanya kampeni kwa ustadi na kupiga kura ili               kuhakikisha kwamba Chama kinapata ushindi wakati wa uchaguzi.

      (p) Kutathmini maendeleo ya Kata/Wadi na kutoa msimamo na mapendekezo ya Chama kwa wanaohusika.

      (q) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama ya Kata/Wadi.

      (r) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya kila mwaka ya maendeleo ya kila kitengo cha Chama.

      (s) Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

      (t) Kamati ya Kata/Wadi itafanya angalau kikao kimoja katika kila miezi mitatu.

(4) Kazi ya Mwenyekiti wa Kata/Wadi:

       (a) Atakuwa msimamizi Mkuu wa shughuli za kila siku za Chama katika Kata/Wadi.

       (b) Atakuwa msemaji na mhamasishaji Mkuu wa Chama katika Kata/Wadi.

       (c) Ataongoza mikutano ya Kata/Wadi.

(5) Kazi ya Katibu wa Kata/Wadi:

       (a) Atakuwa mtendaji Mkuu wa Chama katika Kata/Wadi.

      (b) Atatunza orodha ya Matawi, idadi ya Mashina na Vitongoji na wanachama wa kila Tawi lililoko katika                             Kata/Wadi hiyo.

     (c) Atatunza kumbukumbu za mali za Chama zisizoondosheka na zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ys Kata/Wadi hiyo.

     (d) Atakuwa mdhibiti Mkuu wa mali zaChama katika Kata/Wadi.

     (e) Atawajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika Kata/Wadi kwa ngazi ya Jimbo.

      (f) Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya Chama.

      (g) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa pengine katika katiba hii.

(6) Kazi ya Mweka Hazina wa Kata/Wadi:

       (a) Atabuni/ atatafuta fedha kwa ajili ya Chama.

       (b) Ataweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya Chama.

       (c) Ataandaa bajeti ya Chama.

      (d) Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya Chama.

21. Jimbo.

(1)  Jimbo litakuwa na vikao vifuatavyo:-

        (a) Mkutano Mkuu wa Jimbo.

        (b) Kamati ya Utendaji ya Jimbo.

(2) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo:-

         (a) Mwenyekiti wa Jimbo.

        (b) Katibu wa Jimbo.

        (c) Mweka Hazina wa Jimbo.

       (d) Wenyeviti na Makatibu wa Kata/wadi.

       (e) Mbunge aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

       (f) Mwakilishi aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

      (g) Meya au Naibu Meya au Mwenyekiti, au Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jiji au Manispaa au Mji au Wilaya au Mwenyekiti na Katibu wa Madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

       (h) Madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

       (i) Wenyeviti na Makatibu wa vitengo vya Chama katika Jimbo hilo.

       (j) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wanaoishi katika Jimbo hilo watakuwa waalikwa.

(3) Kazi za Mkutano wa Jimbo:

       (a) Kumchagua Mwenyekiti wa Chama wa Jimbo.

      (b) Kupima utekelezaji wa shughuli za Chama za Jimbo.

       (c) Kutathmini maendeleo ya Jimbo hilo.

       (d) Kutoa mikakati na miongozo kwa ajili ya maendeleo ya Chama katika Jimbo hilo.

      (e) Mkutano Mkuu wa Jimbo utafanyika angalau mara moja katika kila miaka miwili na nusu.

(4) Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jimbo:

        (a) Mwenyekiti wa Jimbo.

       (b) Katibu wa Jimbo

      (c) Mweka hazina wa Jimbo

      (d) Mbunge aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo.

      (e) Mwakilishi aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

     (f) Meya au Naibu Meya au Mwenyekiti au makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jiji au Manispaa au Mji au Wilaya au Mwenyekiti na Katibu wa Madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika Jimbo hilo.

      (g) Wenyeviti na Makatibu wa Jimbo hilo wavitengo vya Chama.

       (h) Wenyeviti wa Kata/Wadi wa Chama wa Jimbo hilo.

      (i) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wanaoishi katika jimbo hilo watakuwa waalikwa.

(5) Kazi za Kamati ya Utendaji wa Jimbo

        (a) Kuunda Sekretarieti ya Chama ya Kamati ya Utendaji ya Jimbo.

        (b) Kukisimika Chama katika jamii kwenye Jimbo.

       (c) Kutekeleza sera na kazi za Chama katika Jimbo hilo.

      (d) Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato ya Chama katika Jimbo hilo.

      (e) Kuweka daftari la orodha za wanachama na viongozi wa Chama katika Jimbo.

      (f) Kutathmini maendeleo katika Jimbo hilo na kutoa msimamo na mapendekezo kwa wanaohusika.

      (g) Kumchagua Mweka Hazina wa Jimbo.

       (h) Kubuni mikakati ya kuhsmasisha watu kwa shabaha ya kuungwa mkono.

      (i) Kujadili au kupendekeza wanaoomba kugombea Ubunge au Uwakilishi na kupeleka mapendekezo kwa                          Halmashauri Kuu ya Taifa.

     (j) Kujadili na kupendekeza wanaoomba kugombea uongozi wa Chama ngazi za Jimbo na Taifa na kupeleka                       mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

       (k) Kujadili maombi na kuteua wagombea uongozi wa Chama ngazi ya Kata/Wadi.

       (l) Kujadili maombi na kuteua wagombea udiwani katika Jimbo hilo.

       (m) Kuhakikisha kwamba wakati wa uchaguzi, kampeni inafanywa kwa ustadi na Chama kinapata ushindi.

      (n) Kujadili na kupitisha uamuzi juu ya maombi ya waliojizulu au kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa waliofukuzwa kujiunga tena na Chama.

     (o) Kuwaondoa madarakani viongozi  wa ngazi ya Kata/Wadi kwa sababu za kukiuka Katiba, kanuni, maadili, nidhamu na sera za Chama.

      (p) Kujadili na kuamua rufaa za wanachama na viongozi kutoka ngazi za chini.

      (q) Kuchunguza mwenendo wa viongozi na wanachama katika Jimbo hilo na kutoa adhabu pale ambapo hapana budi isipokuwa kufukuza uanachama.

       (r) Kuelekeza na kusimamia maandalizi ya umma kwa ajili ya uchaguzi ili kukipatia Chama ushindi.

       (s) Kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jimbo.

     (t) Kuwajibika na kutuma kwa ngazi ya Taifa taarifa za kila mwezi kuhusu utekelezaji wa shughuli za Chama katika Jimbo.

        (u) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama ya jimbo.

       (v) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa  ya kila mwaka ya maendeleo ya vitengo vya Chama.

       (w) Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

       (x) Kamati ya Utendaji ya Jimbo itafanya angalau kikao kimoja katika kila miezi mitatu.

(6) Kazi ya Mwenyekiti wa Jimbo:

        (a) Atakuwa msimamizi Mkuu wa shughuli za kila siku za Chama katika Jimbo hilo.

       (b) Atakuwa msemaji na mhamasishaji Mkuu wa Chama wa Jimbo.

       (c) Ataongoza mikutano ya Jimbo.

(7)  Kazi za Katibu wa Jimbo:

       (a) Atakuwa mtendaji Mkuu wa Chama katika Jimbo.

       (b) Atatunza orodha ya Kata/Wadi, Matawi, Vitongoji, idadi ya Mashina na wanachama wa Jimbo hilo.

     (c) Atatutanza kumbukumbu za mali za Chama zisizoondosheka na zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya Jimbo hilo.

     (d) Atakuwa mdhibiti Mkuu wa mali za Chama wa Jimbo.

    (e) Atawajibika kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika Jimbo kwa ngazi ya Taifa.

   (f) Katika Wilaya yenye Majimbo zaidi ya moja, Katibu wa Chama wa Jimbo yalimo Makao Makuu ya Serikali au taasisi au asasi ya Wilaya, atakuwa kiungo kati ya Chama na Serukali au taasisi au asasi wilayani humo.

     (g) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

(8) Kazi za Mweka Hazina wa Jimbo:

      (a) Atabuni/atatafuta fedha kwa ajili ya Chama.

      (b) Ataweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya chama.

      (c) Ataandaa bajeti ya Chama.

     (d) Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya Chama.

22. Taifa

(1) Kutakuwa na vikao vifuatavyo katika ngazi ya Taifa:-

        (a) Mkutano Mkuu wa Taifa.

       (b) Halmashauri Kuu ya Taifa.

(2) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

       (a) Mwenyekiti wa Taifa.

       (b) Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Tanzania Bara).

       (c) Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Tanzania Zanzibar).

       (d) Katibu Mkuu.

       (e) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara)

       (f) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar).

       (g) Mweka Hazina wa Taifa.

       (h) Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

       (i) Maspika wa Bunge la Afrika, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Jumuiya ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar waluochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

        (j) Rais na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

       (k) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (l) Wajumbe wa Baraza la Wadhamini la Chama.

       (m) Makamu Mkuu wa Chuo cha Chama.

       (n) Wenyeviti wa Chama wa Majimbo.

       (o) Wenyeviti wa Taifa na Makatibu Wakuu wa vitengo vya Chama.

       (p) Wenyeviti na Makatibu wa Wabunge wa Bunge la afrika, bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

(3) Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa:

         (a) Kumchagua Mwenyekiti wa Chama wa Taifa.

         (b) Kumchagua Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Chama wa Taifa kwa ajili ya Tanzania Bara na Makamu                      Mwenyekiti wa Chama wa Taifa kwa ajili ya Tanzania Zanzibar.

        (c) Kuwachagua wajumbe wanaume kumi na watano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao kati yao kumi kutoka Tanzania Bara na Watano watatoka Tanzania Zanzibar.

        (d) Kuwachagua wajumbe wanawake kumi na watano wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ambao kati yao kumi kutoka Tanzania Bara na watano kutoka Tanzania Zanzibar.

        (e) Kuwachagua wajumbe vijana wane wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

        (f) Kuwachagua wajumbe watatu wa kuwakilisha makundi maalumu katika Halmashauri Kuu ya Taifa.

       (g) Wajumbe kutoka kila Mkoa kupendekeza kwa Halmashauri Kuu ya Taifa majina yasiyopungua mawili na kutozidi matatu likiwemo angalaumoja la mwanamke, kwa ajili ya uteuzi wa Kamishna wa Chama wa Mkoa.

       (h) Kubadilisha/kurekebisha Katiba ya Chama.

        (i) Kuteua wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kutokana na mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (j) Kusikiliza na kutolea uamuzi wa mwisho rufaa kutokana na maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

       (k) Kupokea, kutafakari, kubadili au kukataa taarif ya kazi za Chama itakayotolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (l) Kutoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa itikadi, sera na malengo ya Chama.

       (m) Kumwondoa madarakani kwa mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kiongozi yeyote kwa kura zaidi ya nusu ya wajumbe halali waliohudhuria.

        (n) Kutoa uamuzi wa mwisho juu ya jambo lolote linalohusu Chama ambalo halijatajwa jatika Katiba hii.

     (o) Mkutano Mkuu wa Taifa utafanyika kila baada ya miaka mitano isipokuwa kama kuna suala la dharura mkutano maalum wa Taifa unaweza kuitishwa kwa agizo la Halmashauri Kuu ya Taifa.

(4) Wajumbe wa Halmahauri Kuu ya Taifa:

        (a) Mwenyekiti wa Taifa.

        (b) Makamu Mwenyekiti wa Tiafa (Tanzania Bara)

        (c) Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Tanzania Zaanzibar).

       (d) Katibu Mkuu.

       (e) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara).

       (f) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar).

       (g) Mweka Hazina wa Taifa.

       (h) Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama

     (i) Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

       (j) Rais na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

      (k) Maspika wa Bunge la Afrika, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

      (l) Wajumbe wanaume kumi na watano; kumi kutoka Tanzania Bara na watano kutoka Tanzania Zanzibar.

      (m) Wajumbe wanawake kumi na watano; kumi kutoka Tanzania Bara na watano kutoka Tanzania Zanzibar.

      (n) Wenyeviti wa Taifa na Makatibu Wakuu wa vitengo vya Chama.

      (o) Wajumbe kumi walioteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa.

      (p) Wajumbe wane vijana kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

      (q) Wajumbe watatu wa kuwakilisha makundi maalum.

      (r) Makamishna wa Chama wa Mikoa.

      (s) Makamu Mkuu wa chuo cha Chama.

      (t) Wenyeviti na Makatibu wa Wabunge wa Bunge la Afrika, Bunge la Jumuiya ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

(5) Kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa:

         (a) Kumchagua Katibu Mkuu kutoka miongoni mwa wanachama.

        (b) Kumchagua Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara) na Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar) kutoka                              miomgoni mwa wanachama.

        (c) Kumchagua Mweka Hazina wa Taifa kutoka miongoni mwa wanachama.

        (d) Kuteua, kubadilisha, kusimamisha na kuondoa Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini la Chama.

        (e) Kuteua, kupanga, kuhamisha, kubadilisha, kusimamisha na kuondoa Makamishna wa Chama wa Mkoa.

        (f) Kuteua na kuondoa Makatibu wa Majimbo kutokana na mapendekezo ya Katibu Mkuu.

       (g) Kujadili na kupendekeza kwa Mkutano Mkuuwa Taifa wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Zanzibar kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

       (h) Kujadili na kuteua wagombea uongozi wa Chama wa ngazi za Jimbo, Taifa, Ubunge, Uwakilishi,                                        Uspika/Unaibu Spika, Umeya na Uenyekiti wa Halmashauri kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

         (i) Kumvua mwanachama uanacham, au kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu rufaa ya wanachams au kuhusu                          uanachama au uongozi yaliyoletwa mbele yake na kikao cha chini au mwanachama.

         (j) Kutoa uamuzi wa mwisho juu ya maombi ya wanachama, wanaojiunga upya na Chama baada ya kufukuzwa                   uanachama.

         (k) Kupanga shughuli za Chama na kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

         (l) Kutunga sera za Chama kuhusu uchumi na maendeleo ya jamii.

        (m)  Kutekeleza sera za Chama kama zilivyopitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

        (n) Kufuatilia mkoa hadi Mkoa kuhakikisha kwamba, sera za Chama zinatekelezwa kikamilifu na kuwa na matokeo yaliyokusudiwa.

         (o) Kutathimini utekelezaji wa shughuli zote za Chama nchini.

        (p) Kupokea na kuchambua taarifa ya mapato na matumizi ya Chama ya mwaka uliopita na taarifa ya wakaguzi wa hesabu za Chama.

         (q) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya kila mwaka ya maendeleo ya kila kitengo cha Chama.

         (r) Kuweka kanuni na taratibu kuhusu vifaa, fedha, uchaguzi, uajiri, nidhamu, uenezi, vitengo na mambo mengine ambayo itaona inafaa kuyawekea kanuni na taratibu.

         (s) Kutunga ilani ya uchaguzi ya Chama.

        (t) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya kila mwaka ya kazi ya Baraza la Wadhamini la Chama.

         (u) Kupanga kiingilio, ada za Chama na michango ya Kitaifa kwa shughuli mbali mbali za Chama.

        (v) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa Taifa mabadiliko/marekebisho ya Katiba ya Chama.

       (w) Kuonya, kusimamisha au kuondoa madarakani kiongozi yeyote wa Chama wa ngazi ya Taifa na Jimbo na kiongozi wa kitengo cha Chama wa ngazi ya Taifa, isipokuwa kuwaondoa madarakani Mwenyekiti wa Taifa na Makamu Wenyeviti wa Taifa, iwapo mhusika atakiuka Katiba ya Chama, atakuwa mtovu wa nidhamu au atakuwa na mwenendo mbaya.

      (x) Kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Wenyeviti wa Taifa au kiongozi yeyote wa Taifa                         anayewajibika kwa Mkutano Mkuu waTaifa iwapo muhusika atakiuka katiba ya Chama, atakuwa mtovu wa nidhamu au atakuwa na mwenendo mbaya.

      (y) Kujadili na kupitisha bajeti ya Chama ya Taifa.

      (z) Halmashauri Kuu ya Taifa itakutana angalau mara moja kila baada ya miezi sita.

(6) Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa:

         (a) Kitakuwa chombo cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (b) Itafanya kazi yake kwa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (c) Itawajibika kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

       (d) Itafanya kazi zake katika eneo la Tanzania Zanzibar.

      (e) Makamu Mwenyekiti (Tanzania Zanzibar) atakuwa Mwenyekiti wa kikao na Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar) atakuwa Katibu wa kikao.

(7) Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa:

        (a) Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Tanzania Zanzibar).

        (b) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar).

        (c) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa toka Tanzania Zanzibar.

       (d) Mwenyekiti/ Makamu Wenyeviti/ Makatibu Wakuu wa Taifa wa vitengo vya Chama kutoka Tanzania Zanzibar.

        (e) Rais na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

     (f) Spika na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mwenyekiti na Katibu wa Wajumbe wa Baraza la                             Wawakilishi na Mwenyekiti na Katibu wa Bunge la Afrika, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki au Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka Zanzibar waliochaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

(8) Kazi za Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa:

         (a) Kuunda Sekretarieti chini ya Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar).

         (b) Kumchagua Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

         (c) Kumchagua Mweka Hazina (Tanzania Zanzibar).

        (d) Kutekelea shughuli za Chama katika Tanzania Zanzibar

        (e) Kutekeleza sera za Chama kama zilivyopitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

        (f) Kuweka ufuatiliaji wa kutosha Mkoa hadi Mkoa kuhakikisha kwamba kazi za Chama zinatekelezwa kikamilifu na kuwa na matokeo yaliyokusudiwa.

        (g) Kutathmini utekelezaji wa shughuli zote za Chama katika Tanzania Zanzibar.

        (h) Kubuni, kujenga na kudumisha uhusiano mwema kati ya Chama na wananchi na kuwaelimisha juu za sera, malengo na mwelekeo wa Chama.

        (i) Kujadili na kutoa maoni kwa Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya wanachama wanaoombs kugombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

        (j) Kufanya kazi nyingine yoyote kwa maagizi na maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

        (k) Kujadili na kupitisha bajeti ya ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama

        (l) Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya kikao angalau mara moja katika kila miezi sita.

SURA YA SITA
SEKRETARIETI YA CHAMA

23.     Sekretarieti ya Chama;

(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Chama katika kila ngazi; za Taifa, Jimbo, Kata/Wadi na Tawi.

(2) Katika ngazi ya Taifa kutakuwa na Sekretarieti katika Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam na katika ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.

(3) Sekretarieti ya kila ngazi itakuwa na idara zifuatazo:-

          a. Idara ya Organaizesheni na Utawala

          b. Idara ya Fedha, Uchumi na Mapato

          c. Idara ya Itikadi, Sera, Utafiti na Mafunzo

         d. Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma

         e. Idara ya Ulinzi na Usalama

         f. Idara ya Mambo ya nje ya Chama

         g. Idara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu

         h. Idara ya Kampeni na Uchaguzi

         i. Idara ya Taasisi za dola na Vyombo vya Uwakilishi

(4) Sekretarieti itafanya kazi za Chama za utendaji za siku hadi siku.

(5)  Sekretarieti itaundwa mara baada ya wajumbe wa kikao cha kiutendaji cha ngazi husika kuchaguliwa.

(6) Sekretarieti itaundwa kwa kikao cha kiutendaji cha ngazi husika kuidhinisha majina ya wakuu wa idara za Sekretarieti, yatakayokuwa yamependekezwa na Katibu wa Chama wa ngazi hiyo na wakuu wa idara hao ndio watakuwa wajumbe wa Sekretarieti.

(7) Katibu wa Chama atakuwa kiongozi wa Sekretarieti ya ngazi yake, atakuwa na uwezo wa kupanga na kupangua wajumbe wa Sekretarieti na hata kuwaondoa.

(8) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara/ Tanzania Zanzibar) atakuwa Katibu wa vikao vya Sekretarieti ya Chama ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(9) Katibu wa ngazi husika ataweza kuunda idara za Sekretarieti kulingana na mahitaji ya ngazi hiyo.

(10) Sekretarieti za ngazi za Jimbo, Kata/wadi na Tawi zitachagua Makatibu wao mara baada ya kuundwa.

(11) Mweka Hazina wa Chama atakuwa mjumbe wa Sekretarieti ya ngazi ya Chama aliyomo.

(12) Itafanya angalau kikao kimoja kila mwezi.

24.     Sekretarieti ya Chama ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa:

(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Chama ya Kamati Maalum ya Halmashzuri Kuu ya Taifa.

(2) Itakuwa na Idara zilizotajwa katika ibara ndogo ya (3) ya ibara ya 23.

(3) Itafanya kazi za Chama za utendaji za siku hadi siku (Tanzania Zanzibar) kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(4) Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara) atakuwa kiongozi wa Sekretarieti.

(5) Katibu wa vikao vya Sekretarieti atateuliwa na Kamati na mapendekezo ya Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Zanzibar).

SURA YA SABA
VITENGO VYA CHAMA

25.     Vitengo vya Chama.

(1) Chama kitakuwa na vitengo vifuatavyo:

          (a) Kitengo cha Wazee

          (b) Kitengo cha Wanawake

          (c) Kitengo cha Vijana

(2) Vitengo vya Chama vitakuwa chini ya uongozi wa Chama wa ngazi husika na vitawajibika kwa ngazi hiyo kupitia kwa Katibu wa Chama wa ngazi hiyo.

(3) Katibu Mkuu ataandaa kanuni za kusimamia uendeshaji wa shughuli za vitengo na kanuni hizo zitaanza kutumika baada ya kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

(4) Majina ya wagombea kiti cha Mwenyekiti wa Taifa na kiti cha Makamu Wenyekiti wa Taifa wa kila kitengo yatajadiliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

(5) Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu wa kila kitengo watateuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kutokana na majina yasiyopungua mawili na kutozidi matatu likiwemo angalau moja la mwanamke (isipokuwa kitengo cha wanawake majina yotr yatakuwa ya wanawake) kwa kila kiti yatakayo pendekezwa na Kamati ua Utekelezaji ya           Taifa ya kitengo husika.

(6) Majina ya wagombea kiti cha mwenyekiti wa kila kitengo wa Tawi au Kata/wadi au Jimbo yatajadiliwa na kupitishwa na kikao cha kiutendaji cha Chama cha ngazi ya kitengo husika.

(7) Kila kitengo kitatoa taarifa ya utendaji/ maendeleo yake ya kila mwaka kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

SURA YA NANE
BARAZA LA WADHAMINI LA CHAMA

26.     Baraza la Wadhamini la chama

(1) Wajumbe wa Baraza la Wadhamini:

         (a) Mwenyekiti wa Baraza.

        (b) Katibu wa Baraza

        (c)  Wajumbe Watano akiwemo angalau mwanamke mmoja.

(2) Mamlaka na uwezo wa Baraza la Wadhamini.

        (a) Baraza litakuwa na mamlaka na uwepo wa kuyatumia mamlaka yake kama alivyopewa na sheria ya                                 Wadhamini.

       (b) Baraza litafanya kazi zake chini ya usimamizi na maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa na litatoa taarifa ya shughuli zake kwake.

        (c) Mdhamini atakuwa kwenye nafasi ya udhamini kwa muda wa miaka mitano na anaweza kuteuliwa kuendelea na nafasi hiyo baada ya kipindi chake kumalizika.

         (d) Mweka Hazina wa Taifa atakuwa Katibu wa Baraza la wadhamini.

          (e) Baraza litafanya kikao angalau mara moja katika miezi mine.

(3) Mdhamini anaweza kuondolewa katika Baraza na Halmashauri Kuu ya Taifa ikiwa:

         (a) Atakuwa na afya mbaya kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake.

         (b) Ataonekana uwezo mdogo katika kutekeleza majukumu yake.

         (c) Ataishi nje ya nchi kwa miaka miwili mfululizo.

        (d) Atakuwa amekiuka Katiba na maadili ya Chama.

      (e) Atapatikana na hatia ya kosa ambalo Halmashauri Kuu ya Taifa itaridhika kuwa halikustahili kufanywa na Mdhamini wa Chama.

        (f) Atafilisiwa kwa kushindwa kujikomboa katika kipingi cha miezi sita.

(4) Mdhamini atajiuzulu kutoka katika Baraza kwa kutoa tamko la maandishi kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia kwa Mwenyekiti wa Baraza.

(5) Iwapo itatokea nafasi wazi kutokana na kifo, kujiuzulu au kufukuzwa kwa mdhamini, nafasi hiyo itajazwa mara moja kufuarana na taratibu za Katiba hii na sheria inayotumika.

(6) Iwapo Mwenyekiti wa Baraza atashindwa kuhudhuria vikao, wajumbe watamchagua mmojawapo kati yao kuwa Mwenyekiti wa kikao cha siku hiyo.

(7) Kazi za Baraza la Wadhamini;

           (a) Kuweka chini ya uangalizi wake mali zote za Chama zinazoondosheka na zisizoondosheka.

          (b) Kuingia katika shughuli zozote za uvhumi ambazo zinaendana na madhumuni na malengo ya chama kwa kibali cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

         (c) Kuunda Kamati ndogo ndogo na kukasimu kwa kamati hizo madaraka yake ya utendaji na utekelezaji wa baadhi ya shughuli zake.

          (d) Kutoa taarifa ua utendaji ya mwaka katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

       (e) Bila ya kuathiri masharti ya sheria na kanuni za Baraza la Wadhamini, Baraza linaweza kuitisha mkutano maalum pale itakapolazimu kufanya hivyo.

SURA YA TISA
VIONGOZI WAKUU WA CHAMA NA KAZI ZAO

27. Viongozi Wakuu wa Chama na kazi zao;

(1) Viongozi Wakuu:

         (a) Mwenyekiti wa Taifa,

         (b) Makamu Mwenyekiti wa Taifa – Tanzania Bara

         (c) Makamu Mwenyekiti wa Taifa – Tanzania Zanzibar,

        (d) Katubu Mkuu.

        (e) Naibu Katibu Mkuu – Tanzania Bara.

        (f) Naibu Katibu Mkuu – Tanzania Zanzibar

        (g) Mweka Hazina wa Taifa.

(2) Mwenyekiti wa Taifa

        (a) Atakuwa Msemaji Mkuu wa Chama.

       (b) Atakuwa ndiye mhamasishaji Mkuu wa Chama.

       (c) Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa

      (d) Atakuwa Mkuu wa Chuo cha Chama

       (e) Atakuwa na uwezo wa kuteua wajumbe kumi wa kuingia katika Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya                                kushauriana na Katibu Mkuu.

      (f) Atakuwa na uwezo wa kuteua Makamishna wa Chama wa Mikoa kujaza nafasi zilizowazi baada ya uchaguzi mkuu wa Chama na kabla ya uchaguzi mkuu wa Chama unaofuata.

      (g) Atakuwa na uwezo wa kutengua ujumbe wa aliowateua kuingia katika Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya                     kushauriana na Katibu Mkuu.

       (h) Iwapo Mwenyekiti wa Chama wa Taifa hayupo kwa sababu yoyote ya kikazi au ya muda, Makamu Mwenyekiti wa Chama (Tanzania Bara) atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama Taifa, na Makamu Mwenyekiti (Tanzania                 Zanzibar) atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama wa Taifa iwapo Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara)                          atakuwa hayupo.

        (i) Iwapo kiti cha Mwenyekiti wa Chama wa Taifa kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondo uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu ulioelezwa katika (h) ys ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu maalumu wa Taifa unaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho, ili kumchagua Mwenyekiti wa Chama wa Taifa mwingine.

      (j) taweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa litakaloungwa mkono na theluti mbili ya kura za wajumbe halali walioudhuria na kupiga kura.

(3) Makamu Wenyeviti wa Taifa.

          (a) Makamu Mwenyekiti atakayetoka Tanzania Zanzibar atafanya zaidi shughuli za Chama Tanzania Zanzibar na atakayetoka Tanzania Bara atafanya zaidi shughuli za Chama Tanzania Bara.

            (b) Watakuwa wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa Taifa.

            (c) Wataweza kuondolewa kwenye madaraka baada mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la                    Mkutano Mkuu wa Taifa kwa zaidi ya nusu ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.

           (d) Watahusika zaidi na shuguli za uhamasishaji na kampeni za Chama na majukumu mengine watakayopewa na Mwenyekiti wa Chama wa Taifa.

(4) Katibu Mkuu.

              (a) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Chama

             (b) Atakuwa katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

            (c) Atakuwa na uwezo wa kuajiri, kuhamisha, kufukuza, na kusimamia nidhamu ya watendaji/ watumishi wote wa Chama kwa mujibu wa Katiba, kanuni, tarayibu za Chama na sheria za nchi.

             (d) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.

(5) Naibu Makatibu Wakuu.

            (a) Mmoja wapo atamsaidia Katibu Mkuu na kukaimu kiti chake wakati Katibu Mkuu hayupo.     

            (b) Watafanya kazi nyingine zote za Chama watakazopewa na Katibu Mkuu.

            (c) Naibu Katibu Mkuu kutoka Tanzania Zanzibar atafanya zaidi shughuli zake huko Tanzania Zanzibar na                         anaetoka Tanzania Bara atafanya zaidi shughuli zake za Chama Tanzani Bara.

            (d) Watafanya kazi zozote zitakazokuwa zimetajwa penginepo katika Katiba hii.

(6) Mweka Hazina wa Taifa.

            (a) Atakuwa katibu wa Baraza la Wadhamini.

            (b) Atadhibitisha mapato na matumizi ya fedha za Chama.

           (c) Ataandaa bajti ya Chama.

SURA YA KUMI
WAGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA

28. Masharti kuhusu mgombea Urais

(1) Awe ametimiza masharti ya Katiba ya nchi kuhusu mgombea wa kiti cha Urais.

(2) Awe mwanachama wa NCCR-MAGEUZI mwenye sifa za kuwa kiongozi na awe amejihusisha katika uongozi wa aina yoyote katika jamii.

(3) Aungwe mkono na wanachama wasiopungua mia mbili.

(4) Awe anaelewa na kuishi katika Katiba na sera za Chama.

(5) Atateua kwa kushirikiana na Halmashauri Kuu ya Taifa, mwanachama wenye sifa zinazokubalika kichama kuwa mgombea mwenza akati wa kampeni za Urais.

(6) Iwapo mgombea Urais atashinda, basi atalazimika kusimamia utekelezaji wa sera za Chama serikalini.

(7) Isipokuwa kwa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, masharti haya yanamuhusu pia mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

SURA YA KUMI NA MOJA
MAMBO YA JUMLA KUHUSU CHAMA

29. Uchaguzi

(1) Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Chama utafanyika kila baada ya miaka mitano au vinginevyo kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa.

(2) Katika uchaguzi wa kila ngazi ya uongozi kuanzia Shina hadi Jimbo, utasimamiwa na ngazi ya juu yake na ngazi ya Taifa itasimamiwa na utaratibu utakaowekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

(3) Ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na aliyekuwa ameshikilia nafasi hiyo kujiuzulu au kufariki au kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba hii, uchaguzi unaweza kufanyika wakati wowote bils kungoja kipindi cha miaka mitano cha uongozi uliopita katika Chama kupita.

(4) Uchaguzi wa Chama wa ngazi zote utakuwa kwa kura za siri.

(5) Iwapo nafasi ya mjumbe wa Hal,mashauri kuu ya Taifa utakuwa wazi kwa sababu yoyote ile, Halmashauri kuu ya Taifa itaweka utaratibu wa kujaza nafasi hiyo.

(6)     Wakati wa mkutano wa uchaguzi, mmoja wa wajumbe ambaye siyo mgombea, atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda wa kuongoza mkutano huo.

30. Akidi ya vikao:

Akidi ya kila kikao cha Chama itakuwa nusu ya wajumbe halali wa kikao hicho isipokuwa pale ilipoelekezwa vinginevyo na Katiba hii.

31. Uitishaji wa vikao

(1) Kila kikao cha Chama kitaitishwa na Katibu baada ya kushauriana na kukubaliana na Mwenyekiti wa kikao hicho.

(2) Vikao vya mikutano mikuu ya Taifa na jimbo vya kawaida vitaitishwa kwa taarifa ya siku zisizopungua ishirini na moja.

(3) Kikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa, Kamati ya Utendaji ya Jimbo, Kamati ya Kata/wadi na Mkutano Mkuu wa Tawi vitaitishwa kwa taarifa ya siku zisizopungua kumi na nne.

(4) Vikao vya kawaida vya Kamati ya Tawi, Kiongoji na Mkutano wa Shina vitaitishwa kwa taarifa ya siku zisizopungua saba.

(5) Muda wa taarifa ya kuitisha kikao chochote kilichotajwa katika ibara ndogo za (2), (3), na (4) za ibara hii unaweza kuwa pungufu ya uliotajwa iwapo kikao kinachoitishwa ni maalum au cha dharura.

32. Mjumbe wa kikao kupoteza sifa:

Mjumbe ambaye hatahudhuria vikao vitatu mfululizo bila udhuru au sababu inayokubalika kwa uongozi unaohusika, atakuwa amejivua ujumbe katika kikao hicho.

33. Ratiba ya vikao;

Kila kikao cha Chama kitafanyika katika muda uliotajwa katika Katiba hii, isipokuwa likitokea jambo maalum au la dharura linalohitaji kikao kifanyike.

34. Vikao kukasimu mamlaka na madaraka:

Kikao chochote cha Chama kinaweza kukasimu kwa azimio, mamlaka na madaraka yake kwa kikao kilicho chini yake.

Katika kufanikisha shughuli zake kikao chochote cha Chama kinaweza kuunda kamati au tume kwa ajili hiyo na kutoa hadidu za rejea zinazohusu jambo hilo.

35. Kukaimu madaraka

(1) Iwapo mwanaxhama au kiongozi yeyote, kwa sababu yoyote ile hawezi kutekeleza kazi zake kwa muda au amesimamishwa au amevuliwa madaraka kwa mijibu wa Katiba, kanuni na taratibu za Chama, mamlaka iliyo na uwezo wa uchaguzi au uteuzu wa nafasi hiyo, inaweza kumteua mwanachama mwenye sifa zinazohitajika kukaimu nafasi hiyo ya uongozi iliyowazi.

(2) Kukaimu madaraka kutakoma mara tu mtu aliyekaimiwa atakaporudi katika nafasi yake au mwanachama mwingine kuchaguliwa au kuteuliwa kujaza nafasi hiyo na kwa vyovyote vile kukaimu madarakahakutazidi kipindi cha miezi sita bila ya nafasi hiyo kujazwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, isipokuwa pale Halmashauri kuu ya Taifa itakapokuwa imeamua au kuelekeza vinginevyo.

36. Kura za uamuzi:

(1) Uamuzi wowote utafikiwa kwa kuungwa mkono na zaidi ya nusu ya kura zote za wajumbe halali waliohudhuria kikao isipokuwa pale ilipoelekezwa vinginevyo na Katiba hii.

(2)  Mwenyekiti wa kikao atakuwa na kura ya uamuzi iwapi pande mbili zitakuwa na kura zinazolingana.

37. Uchaguzi/ uteuzi wa Makamishna wa Chama wa Mikoa na Kazi zao:

(1)  Kutakuwa na Kamishna wa Chama katika kila Mkoa.

(2) Watateuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kutokana na majina yasiyopungua mawili wala kuzidi matatu, kutoka kila Mkoa yaliyopendekezwa na kupigiwa kura na wajumbe wa Mikoa yao wakati wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

(3) Watapangiwa vituo vyao vya kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa.

(4) Watawakilisha Chama katika shughuli za kimkoa za Chama na za nje ya Chama.

(5) Watakuwa wanawasilisha Majimboni mambo watakayotumwa na ngazi ya Taifa na kuwasilisha Taifani mambo watakayotumwa na Majimbo ya Mikoa yao.

(6) Watatekeleza majukumu maalum ya kisiasa na kiutendaji kwa mujibu wa ,maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(7) Endapo nafsi ya Kamishna wa Chama wa Mkoa itakuwa wazi katika wakati ambao siyo wa uchaguzi Mkuu wa Chama, nafasi hiyo itajazwa na Mwenyekiti wa Chama wa Taifa kwa kuteua jina mojawapo ya yale ambayo hayakuteuliwa, baada ya kupendekezwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kutoka Mkoa husika au vinginevyo kwa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

38. Uteuzi wa Makatibu wa Chama:

Makatibu wa Chama ngazi zote isipokuwa ngazi ya Taifa watateuliwa kama ifuatavyo:

(1) Makatibu wa Chama wa Mashina na Vitingoji watateuliwa na Kamati ya Chama ya Tawi kutokana na mapendekezo ya Katibu wa Chama wa Tawi.

(2) Makatibu wa Chama wa Matawi watateuliwa na Kamati ya Chama ya Kata/Wadi kutokana na mapendekezo ya Katibu wa Chama wa Kata/Wadi.

(3) Makatibu wa Chama wa Kata/Wadi watateuliwa na Kamati ya Utendaji ya Chama ya Jimbo kutokana na mapendekezo ya Katibu wa Chama wa Jimbo.

(4) Makatibu wa Chama wa Majimbo watateuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kutokana na mapendekezo ya Katibu Mkuu.

39. Utaratibu wa kuzingatia kwa aliyejiuzulu uanachama;

(1) Aliyejiuzulu au aliyefukuzwa uanachama hararejeshewa ada au mchango wowote aliotoa kwa Chama.

(2) Aliyrjiuzulu uanachama anaweza kuwa mwanachama tena kwa kuomba upya uanachama kupitia Tawi lake. Uamuzi wa kumruhusu kuwa mwanachama tena utatolewa na Kamati ya Utendaji ya jimbo baada ya Kamati ya Tawi kuridhika nae.

(3) Aliyefukuzwa kutoka Chama anaweza kuwa mwanachama tena kwa kuomba upya uanachama kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Kamati ya Tawi na Kamati ya Utendaji ya Jimbo ambazo zitatoa mapendekezo ya kuridhika au kutoridhika na mwnendo wake.

(4) Aliyejiuzulu au aliyefukuzwa anaweza kuwa mwanachama tena kwa utaratibu rahisi zaidi kuliko uliotajwa katika ibara ndogo za (6) na (7) za ibara hii iwapo kuna dharura inayohitaji ifanyike hivyo. Dharura itakayokubalika na utataribu huo rahisi utakaofuatwa vitafafanuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama kama itakavyoona inafaa.

(5) Aliejiuzulu au kufukuzwa uanachama atawajibika kurejesha mali au amana za Chama alizonazo.

(6) Aliyejiuzulu au kufukuzwa andapo atakubaliwa kurejea katika Chama atawajibika kununu kasi mpya.

40. Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi:

Kila itakapohitajika Kamati ya Nidhamu na usuluhishi yenye wajumbe watano itaundwa na kila kikao cha Chama cha kiutendaji cha kila ngazi kuanzia Tawi hadi Taifa na itaendesha shughuli zake kwa mujibu wa kanuni za nidhamu na usuluhishi zitakazowekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa. Kamati hii itashughulikia nidhamu ya viongozi wa kuchaguliwa na wanachama tu. Watendaji wa Chama wa kujitolea, kuteuliwa au kuajiriwa watasimamiwa na kanuni za utendaji au ajira zitakazowekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

41. Taasisi, Asasi na Nishani za Chama

(1) Halmashauri Kuu ya Taifa itakuwa na mamlaka ya kuunda taasisi na asasi kwa kadri itakavyoona inafaa kwa masilahi na maendeleo ya Chama ambazo zitakuwa zinajiendesha zenyewe chini ya mamlaka ya chama na kuzivunja panapohitajika kufanya hivyo.

(2) Pasipo kukiuka Katiba ya Chama, Halmashauri Kuu ya Taifa itakuwa na mamlaka ya kuunda nafasi yoyote na kutoa nishani yoyote katika utekelezaji wa malengo, madhumuni, sera na itikadi ya Chama.

42. Mabadiliko/ Marekebisho ya Katiba:

(1) Katiba inaweza kubadilishwa na au kurekebishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kutokana na mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

(2) Mabadiliko au marekebisho yoyote ya Katiba hii yatafanyika kwa akidi ya mahudhurio isiyopungua theluthi mbili ya wajumbe halali wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

(3) Bila kuathiri ibara ndogo ya (2) ya ibara hii ya Katiba, mabadiliko au marekebisho ya Katiba yatakuwa halali kama yatafanwa na kukubaliwa na theluthi mbili ya wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.

43. Chama kuungana na Chama kingine/Vyama vingine;

(1) Chama kinaweza kuungana na Chama kingine/ Vyama vingine kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa iliohudhuriwa na wajumbe halali wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote na azimio hilo kuugwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.

(2) Azimio la kuungana na Chama kingine/ Vyama vingine, litapitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa na kuwasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu maalumu wa Taifa kwa ajili ya kupata idhini ya mwisho.