Vitengo vya Chama

Chama kina vitengo vifuatavyo:

1. Kitengo cha Wazee.

2. Kitengo cha Wanawake.

3. Kitengo cha Vijana.

Vitengo vya Chama viko chini ya uongozi wa Chama wa ngazi husika kupitia kwa Katibu wa Chama wa ngazi hiyo

Katibu Mkuu ataandaa kanuni za kusimamia uendeshaji wa shughuli za vitengo na kanuni hizo zitaanza kutumika baada ya kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Majina ya wagombea kiti cha Mwenyeviti wa Taifa na Makamu Wenyeviti wa Taifa wa kila Kitengo yatajadiliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu wa kila Kitengo watateuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kutokana na majina yasiyopungua mawili na kutozidi matatu likiwemo angalau moja la Mwanamke (isipokuwa kitengo cha Wanawake majina yote yatakuwa ya Wanawake) kwa kila kiti yatakayopendekezwa na Kamati ya Utekelezaji ya Taifa ya Kitengo husika.

Majina ya Wagombea kiti cha Mwenyekiti wa kila kitengo wa Tawi au Kata/Wadi au Jimbo yatajadiliwa na kupitishwa na kikao cha kiutendaji cha Chama cha ngazi ya kitengo husika.

Kila kitengo kinatoa taarifa ya utendaji/maendeleo yake kila mwaka kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.