Pamoja Tutashinda

Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama cha NCCR-MAGEUZI imefanya uchaguzi wa katibu mkuu wa chama

  • Posted by NCCR Habari
  • On October 17, 2016

Jumamosi ya tarehe 15 mwezi wa 10 mwaka 2016, Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama cha NCCR-MAGEUZI imefanya uchaguzi wa katibu mkuu wa chama na kufanikiwa kumchagua Ndugu  Martin Danda Juju aliyepata kura 47 dhidi ya mgombea mwenza Ndugu Faustin Sungura aliyepata kura 24, huku naibu katibu mkuu, Tanzania Bara akichaguliwa kuwa ni Ndugu Elizabeth Mhagama aliyeshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 67 dhidi ya mgombea mwenza Ndugu Hassan Mrage aliyepata kura 4.

 Pia, Ndugu Mike Ayubu Karama alichaguliwa kuwa mweka hadhina wa chama kwa kupata kura 52 dhidi ya mgombea mwenza Ndugu Beati Mpitabakana aliyepata kura 19.

 Katika Uchaguzi huo, wajumbe waliohudhuria na kupiga kura walikuwa 71 na pia waliweza kuwachagua wajumbe wapya watano ambao ni Ndugu Martin Mngo’ngo’, Ndugu azory Nditije Mteko, Mwalimu AnnaJoyce Kalumuna na Ndugu Blandina Msimbe.

0 Comments

Leave Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *